BREAKING: Jeshi la Gabon Lawmpindua Rais wa Nchi hiyo Ali Bongo


Jeshi la Gabon limempindua Rais wa Nchi hiyo Ali Bongo siku kadhaa baada ya Uchaguzi uliomrejesha madarakani, Wanajeshi hao wameongea kupitia Televishion ya Taifa wakisema wameamua kuwalinda Wananchi kwa kuumaliza Uongozi usiofaa ambapo umeingia madarakani kwa kura za wizi.

Wanajeshi 12 wameonekana kwenye televisheni wakitangaza kuwa wanafuta matokeo ya uchaguzi na kuvunja Taasisi zote za Jamhuri.

Taarifa ya Jeshi hilo imesema “Tume ya Uchaguzi wa tarehe 26 Agosti 2023 haikutimiza masharti ya kura ya uwazi ambayo Watu wa Gabon walitarajia, huu ni utawala usio na uwajibikaji na usiotabirika, unaosababisha kuendelea kuzorota kwa mshikamano wa kijamii, na hatari ya kusababisha Nchi katika machafuko, tunafuta matokeo, mipaka imefungwa hadi taarifa zaidi, Taasisi zote za Jamhuto zimevunjwa ikiwemo Seneti, Bunge la Kitaifa, Mahakama ya Katiba, Baraza la Uchumi, Kijamii na Mazingira na Kituo cha Uchaguzi cha Gabon”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad