Rais Samia Apangua Baraza la Mawaziri, Huu Hapa Mkeka Mzima

Rais Samia Apangua Baraza la Mawaziri, Huu Hapa Mkeka Mzima


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri. Katika mabadliko hayo, Rais Samia ameanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu na kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake kuunda wizara mpya mbili ambazo ni; Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.


Aidha, ameimarisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuongeza nafasi ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu watakaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.


Katika mabadiliko hayo, Rais amemteua Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri wanne, Naibu Mawaziri watano, Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuu watatu. Vilevile, amewabadilisha wizara baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu.


Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo; A) Uteuzi wa Naibu Waziri Mkuu: Dkt. Doto Mashaka Biteko ameteuliwa kuwa Naibu na Waziri na Nishati. Katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu, atakuwa anashughulikia Uratibu wa Shughuli za Serikali.


B) Uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri: Jerry William Silaa, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, ameteuliwa kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Antony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, ameteuliwa kuwa Waziri wa Madini.


Prof Makame Mbarawa, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi.


Innocent Bashungwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.


Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.


Alexander Mnyeti, Mbunge wa Jimbo la Misungwi ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.


David Kihenzile, Mbungu wa Jimbo la Mufindi Kusini, ameteuliwa Naibu Waziri wa Uchukuzi.


Judith Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum Ruvuma, ameteuliwa kuwa Naibu Wwaziri wa Nishati na Dunstan Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.


Mawaziri na Manaibu waliohamishwa wizara na uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu wakuu na uhamisho wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad