Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho leo, imepinga kitendo cha polisi kukaa na watuhumiwa hao kwa zaidi ya saa 48 kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 32 kinachowataka polisi kumfikisha mtuhumiwa mahakamani au kumwachia huru ndani ya muda huo.
“Wakili Boniphace Mwabukusu na wenzake wapo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi tangu 11 Agosti, 2023 bila kupelekwa mahakamani,” imeeleza taarifa.
Aidha, chama hicho kimetaka mageuzi ya Jeshi la Polisi katika kuimarisha mfumo wa haki jinai na kuondoa changamoto nyingi ambazo chama kimedai zinapelekea uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.