Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) Waitaka Simba Kuomba Radhi Kisa Simba Day




Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) kwa pamoia na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamelaani vikali kitendo kilichofanywa Aug 06,2023 kwenye Simba Day kumtumia Mtu mwenye Ualbino mithili ya Mtu aliyekuwa katika hali ya nusu utupu na aliyevaa nepi ya mkojo jukwaani, mbele ya kadamnasi ya Maelfu katika Uwanja wa Taifa ambapo wameutaka Uongozi wa Simba SC uombe radhi.

Kupitia taarifa yao ya pamoja Mwenyekiti Taifa wa TAS, Godson Mollel na Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga wamesema “Tukio hili linafuatia tukio jingine lililofanywa na Timu hii mwaka jana Aug 08,2023 kwenye Simba Day ambapo kulitokea kitendo cha kutumia jeneza, msalaba na kumnasibu Mtu mwenye Albino kama Msukule”

“Vitendo hivi vinatweza utu wa Watu wenye Ualbino nchini na vinapelekea kuwepo kwa mijadala mingi katika Jamii ikiwemo mitandaoni inayoonesha dhihaka kwa Watu wenye Ualbino kinyume na Haki za Binadamu”

“Tunautaka Uongozi wa Simba uombe radhi kwa Watu wenye Ualbino na Umma wa Watanzania kwa vitendo hivi vya kutweza utu wa Watu wenye Albino na tunaiomba Serikali na TFF wasimamie jambo hili”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad