Chanzo Chatajwa Kukosa Hamu Tendo la ndoa

Chanzo Chatajwa Kukosa Hamu Tendo la ndoa


Watanzania washauriwa kurudi katika matumizi ya mbegu za asili ili kuondokana na changamoto mbalimbali za kiafya zikiwemo ukosefu wa nguvu za kiume pamoja na kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.


Akizungumza katika maonyesho ya wakulima Nanenane Kanda ya Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo ambapo kumefanyika  maonyesho ya vyakula vya asili katika benki ya mbegu, Tausi Mwachi mkazi wa Mtwara amesema kuwa ulaji wa vyakula vya asili unarejesha heshima ndani ya nyumba.


“Kuna muda mtu unafikia hatua unakosa hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke lakini kwa wanaume nguvu zinapungua tatizo watu wengi wameacha kutumia mbegu za asili ambazo zinafaida kubwa mwilini na virutubisho visivyo ambavyo tumevikosa kwa muda mrefu ambapo unapika na kuweka kuweka chumvi”


RELATED

Watumiaji wa Vega hatarini kupoteza nguvu za kiume

Kitaifa 19 hours ago

Wanaume wadai wanarukishwa kichurachura kupewa tendo la ndoa

Kitaifa 19 hours ago

Mkurugenzi wa Swissaid Tanzania, Betty Malaki amesema kuwa siku ya maonyesho ya vyakula vya asili ni siku muhimu na inahitaji kuenziwa kwa kuwa inatuhusu.


“Ili kuendelea kutunza mbegu za asili tunajaribu kufanya ushawishi kwa jamii ili kuhakikisha kuwa mbegu za asili zinakuwepo na Serikali kuwekeza nguvu katika mbegu za asilia ili mtu achague nini atumie nini apande.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abasi amesema kuwa tunapaswa kula chakula cha asili kilichoandaliwa kiasili kwa ajili ya kuondoa changamoto ya watu kukosa nguvu ikiwemo nguvu za kiume.


“Mbegu za asili ndiyo msingi wa mbegu bora niwapongeze kwa kuadhimisha Siku ya Mbegu. Kama hatukumbushani utamaduni wetu vitu vya asili vitapotea,” amesema Kanal Abass.


Dk John Tenga ambaye ni mtafiti wa mazao kunde na nafaka kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) Kituo cha Naliendele, amesema kuwa mbegu zipo zilizo bora na zinazo himili ukame ambapo zipo ambazo tunazifanyia utafiti ili ziwe bora zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad