Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo upo kwenye mpango wa kuziondoa shule za sekondari za kutwa ili kuongeza ufanisi kwenye elimu.
Akizungumza leo Alhamisi Agosti 31, 2023 wakati wa hafla ya kutambua mchango wa wadau kwenye sekta ya elimu Chalamila amesema suala hilo lipo kwenye vipaumbele vya elimu vya mkoa.
“Vipaumbele vyetu katika mkoa ni kufuta shule za kutwa kwa sekondari ili wanafunzi waweze kufundishwa katika mazingira mazuri.
“Tunataka wanafunzi wote wawe kwenye shule za bweni na hili tutalifanya taratibu tukiamini kwamba tukifanikisha hilo wanafunzi watakuwa katika mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishika,” amesema Chamalamila.
Mkuu huyo wa mkoa amebainisha kuwa kwa sasa mkoa wake unatakeleza miradi ya elimu yenye thamani ya Sh85 bilioni kwa shule za msingi na sekondari.