Diamond aibuka na Harmonize Wasafi Festival 2023

Diamond aibuka na Harmonize Wasafi Festival 2023


Diamond Platnumz, msanii ambaye pia ni mkurugenzi mkuu mtendaji wa lebo ya Wasafi amefunguka kwamba mkoa wa Mtwara, ambao ni nyumbani kwa kina Harmonize ni mkoa ambao una kismati sana na biashara yake ya WCB Wasafi.


Diamond alikumbuka kwamba Mtwara, mkoa ulioko kusini mwa Tanzania, ndio sehemu ambapo alifanya shoo yake ya kwanza kabisa miaka kadhaa iliyopita wakati anatoka kimuziki.


Msanii huyo alisema kwamba shoo aliyoifanya Mtwara ilimtoa kimuziki kipindi hicho wakiwa na Alikiba kwenye tamasha.


Diamond pia alisema wakati aaanzisha lebo ya Wasafi, Mtwara ndio ilimpa msanii wake wa kwanza Harmonize ambaye aliishia kujijenga na kuwa jina kubwa ambalo alikiri hatosita kujivunia.


Diamond alisema kuwa anatarajia tena kupata msanii mwingine kama Harmonize kutoka mkoa huo ili pia amsaini kwenye Wasafi na kuendeleza historia yake nzuri na mkoa huyo, ngome ya Harmonize.


“Wakati tunaanza kufanya lebo msanii wetu wa kwanza tulimtoa Mtwara, na wote mnaona mazuri na makubwa anayoyafanya [Harmonize] na nitafurahi sana kupata msanii Harmonize mwingine kutoka Mtwara kwa sababu ukiangalia pale Wasafi sasa hivi hatuna msanii kutoka Kusini. Kama tuliweza kupata Harmonize kule, hatuwezi kosa kupata Harmonize mwingine pia.


“Nitafurahi sana kama tutakwenda Mtwara na kumpata msanii mwenye talanta tukamsaini tukamtambulisha tukawa tuko na mwakilishi kutoka Mtwara, naye tukamsukuma akafika sehemu fulani akashika naye wenzake mkono kama kaka zake walivyofanya, tutafarijika sana,” Diamond alisema.


Msanii huyo alikuwa anapigia upato tamasha lijalo la Wasafi Festival ambalo linatarajiwa kung’oa nanga katika mkoa huo wa Kusini mwa Tanzania siku chache zijazo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad