Dk. Slaa aachiwa kwa dhamana, Mwabukusi, Mdude kitendawili





HATIMAYE Balozi Dk. Wilbroad Slaa leo Ijumaa mchana ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana aliyoagizwa na Jeshi la Polisi Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu ..(endelea).

Wakili wa mwanasiasa huyo mkongwe, Dickson Matata amethibitisha kuachiwa kwa Dk. Slaa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam baada ya jana usiku kurejeshwa jijini hapa kutokea mkoani Mbeya.

Awali Wakili Matata aliueleza MwanaHALISI Online kwamba polisi walimpigia simu na kumtaka afike kituoni hapo kukamilisha taratobu za dhamana ya mteja wake.

“Polisi wametaka wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kata wanazoishi,” amesema.


Dk. Slaa alikamatwa Jumapili iliyopita nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za uchochezi na uhaini ambazo pia watuhumiwa wengine Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali wanakabiliwa nazo.

Hata hivyo, wote walisafirishwa kupelekwa Mbeya kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka hayo lakini sasa Dk. Slaa jana amerejeshwa Dar es Salaam na kuachiwa kwa dhamana huku hatima ya  watuhumiwa wenzake ikiwa haifahamiki.

Watuhumiwa hao walikmatawa baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillius Wambura wiki iliyopita kuueleza umma kuwa kuna watu wamepanga maandamano yasiyo na kikomo na kutaka kuipindua Serikali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad