Dkt. Slaa, Mwambukusi Wamwangukia Rais Samia Sakata la Kushikiliwa na Polisi

 

Dkt. Slaa, Mwambukusi Wamwangukia Rais Samia Sakata la Kushikiliwa na Polisi

Wakili wa Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mpaluka Nyagali maarufu kwa jina la Mdude Nyagali wanao shikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za Uhaini, amemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la watuhumiwa hao Ili waweze kupelekwa mahakamani na haki iweze kutendeka.


Akizungumza na waandishi wa habari Wakili Philip Mwakilima amesema bado kumekua na vikwazo kwa watuhumiwa Balozi Dkt Wilbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali, kufikishwa mahakamani licha ya kukaa zaidi ya siku tano mahabusu tangu walipokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita,


Pamaoja na hayo Wakili Mwakilima amemuomba Rais Dkt Samia kuingilia kati kwa kutoa amri ya watu hao kufikishwa katika vyombo vya utoaji haki Ili waweze kutoa hakiyao ikiwemo ya matibabu kutokana na wateja wao kua na maradhi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad