Prof. Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma ambapo amesema tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa mitaala hiyo itatangazwa baada ya kupitishwa kwa Sera hiyo na kwamba itakapopitishwa utekelezaji utaanza kwa awamu.
Mkenda amesema rasimu hiyo inapendekeza Watoto waliopo darasa la tatu Mwaka huu 2023 ndio watakaosoma mpaka darasa la sita, hivyo wale waliopo darasa la nne, tano na sita wataendelea kusoma mpaka darasa la saba.
"Hatima ya yote utekelezaji huu unategemea Mamlaka ya Nchi itakaposema tuanze, matumaini yetu ni makubwa kwamba rasimu hii itapita na siku ya kutangazwa kuanza kwa utekelezaji itakuwa ni siku kubwa katika kuelekea mageuzi ya elimu nchini"