Fabrice Ngoma Amtibulia Kanoute Simba Robertinho Afunguka

Fabrice Ngoma Amtibulia Kanoute Simba Robertinho Afunguka


BENCHI la Ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ linafikiria kumuondoa kikosi cha kwanza kiungo mkabaji Sadio Kanoute, ili nafasi yake ichukuliwe na Fabrice Ngoma.


Ngoma raia wa DR Congo, ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu huu ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Jonas Mkude.


Mkongomani huyo anacheza nafasi ya kiungo mkabaji, katika mechi mbili za Ngao ya Jamii, hakuanza huku nafasi yake akicheza Kanoute.



Sadio Kanoute

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameliambia Spoti Xtra kuwa, viongozi wa benchi la ufundi wamegawanyika, wapo wanaotaka Ngoma aanze, wengine wakimuhitaji Kanoute ambaye ameonekana kipenzi cha Robertinho.


Bosi huyo alisema kuwa, upo uwezekano mkubwa wa Ngoma kuingia katika kikosi cha kwanza katika michezo ijayo baada ya kuonesha kiwango bora kila alipotokea benchi wakati wa michezo ya Ngao ya Jamii iliyofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Aliongeza kuwa, kuingia kwa Ngoma akipishwa na Kanoute, alionekana kubadili mchezo na kuituliza safu ya kiungo.


“Katika michezo hii miwili ya Ngao ya Jamii tuliyocheza, itoshe kumuingia Ngoma katika kikosi cha kwanza cha Simba ambacho Kocha Robertinho anaendelea kukisuka kwa ajili ya msimu huu.


“Kocha Robertinho anataka kuendelea kuwaanzisha Kanoute na Mzamiru, lakini viongozi wenzake wa benchi la ufundi walimshauri kumuingiza Ngoma ili wawe mtu mmoja mwenye uwezo wa umiliki wa mpira na kuchezesha timu.


“Hivyo Kanoute huenda akaondoka katika kikosi cha kwanza na kuingia Ngoma, hiyo ni kutokana na Kanoute na Mzamiru aina yao ya uchezaji kufanana, hivyo anahitajika mwingine kuingia kiungo aina ya Ngoma,” alisema bosi huyo.


Akizungumzia hilo, Robertinho alisema: “Kila mchezaji wangu katika timu ana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, nifurahie ushindani uliokuwepo hivi sasa katika timu.”


STORI NA WILBERT MOLANDI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad