Fahyma "Rayvanny ni kila kitu kwangu Ndio Dunia yangu, Hawezi Kubabaishwa na Vitu vya Mtandaoni"

  

Fahyma "Rayvanny ni kila kitu kwangu Ndio Dunia yangu, Hawezi Kubabaishwa na Vitu vya Mtandaoni"

 Fahyma "Rayvanny ni kila kitu kwangu Ndio Dunia yangu, Hawezi Kubabaishwa na Vitu vya Mtandaoni"

Mwanamitindo maarufu Bongo, Fahyma amesema kuwa tayari mzazi mwenzake ambaye ni supastaa wa Bongo Fleva, Rayvanny ameshamtolea mahari na wanategemea kufunga ndoa hivi karibuni.

Fahyma ambaye pia anafahamika kama Fayvanny amesema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na vyombo vya habari hivi karibuni baada ya kurejesha nyumba yake na Vanny Boy iliyokuwa imetetereka baada mzazi mwenzake huyo kunyakuliwa na Paula wa Kajala.


“Tumekuwa wote kwa muda mrefu, kuna zile changamoto za hapa na pale lakini kila kitu kinakwenda sawa. Mume wangu ni kitu cha thamani tosha ukiacha vingine huwa vinakuja tu.


“Mume wangu ni mtu ambaye anajua vitu vingi, amefanya vitu vingi, amekwenda nchi nyingi kwa hiyo hawezi kubabaishwa na maneno ya mtandaoni, sisi kama familia tunajua tunataka kufanya nini na mimi nimekuwa nikimshauri kila mara fanya hiki na kile kwa sababu ndiyo furaha yangu.


“Ninajiamini kumita Rayvanny mume wangu kwa sababu ameshanitolea mahari zamani kidogo, na ni mume wangu na hivi karibuni tutafunga ndoa. Mambo ya dini yanategemea, ikifika huo muda tutajua," amesema Fahyma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad