Faida Ya Kutafuna Mhogo, Nazi Kwa Wanaume! Soma Hapa




MIHOGO na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kinamama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.  Uwezo wa mihogo na nazi mbata au kwa kuchanganya na karanga katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata au karanga. Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kinababa, vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa.

Mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) na karanga ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuimarisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana kwenye vyakula hivyo. Vyakula hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu.

Zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi, karanga na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho. Mihogo mibichi, karanga na nazi mbata husaidia kuimarisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi. Faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi au karanga aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho ‘lauric acid’.

Faida nyingine ya nazi mbata na karanga ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides – MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad