Uamuzi huo umechukuliwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (#FIFA) kutokana na kitendo cha Rais huyo cha kumbusu mdomoni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uhispania, Jenni Hermoso ambaye amesema hakuridhia kitendo kile
Barua ya FIFA kwenda kwa Shirikisho la Soka la Uhispania (#RFEF) kuhusu Rais wa Shirikisho hilo, Luis Rubiales imeeleza kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa kwa kuzingatia Kifungu cha 51 cha Kanuni za Nidhamu za FIFA (FDC), ambapo anatakiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa ngazi ya Kitaifa na Kimataifa wakati suala lake likifanyiwa uchunguzi