Figo ya Nguruwe Yawekwa Katika Mwili wa Binadamu na Kufanya Kazi





Figo ya Nguruwe Yawekwa Katika Mwili wa Binadamu na Kufanya Kazi

Figo ya nguruwe ambayo ilipandikizwa katika mwili wa Binadamu kwa zaidi ya mwezi mmoja, imefanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni hatua ambayo Madaktari wa upasuaji wana matumaini makubwa kwamba siku moja wataweza kutumia aina hii ya upasuaji kuokoa maisha ya Binadamu ambao ni Wagonjwa.

Upasuaji huo wa majaribio ulifanyika kwa idhini ya Familia ya Mtu ambaye alikuwa ametangazwa kuwa ubongo wake hautaweza kufanya kazi tena na kuamua kutoa mwili wake kwa ajili ya tafiti za kisayansi.

Hospitali ya Chuo cha ‘NYU Langone Health’ cha Jijini Newyork nchini Marekani mapema wiki hii kimetangaza kuwa jaribio hili linaashiria muda mrefu zaidi wa figo ya nguruwe iliyotengenezwa kwa vinasaba kufanya kazi ndani ya mwili wa Binadamu.

Mwaka jana, Madaktari wa upasuaji wa Chuo Kikuu cha Maryland waliweka historia kwa kupandikiza moyo wa nguruwe ndani ya Binadamu aliyekuwa anakaribia kupoteza maisha yake ambapo aliweza kuishi kwa muda wa miezi miwili kabla ya moyo huo kuacha kufanya kazi kwasababu ambazo hazieleweki kikamilifu mpaka sasa lakini hatua hiyo inatumika kwa ajili ya mafunzo ya majaribio yajayo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad