Hatimaye Kampuni ya Mziki ya Ziiki Yamjibu Harmonize


Kampuni ya ku-stream muziki ya @mziiki imejibu shutma dhidi ya msanii wa Afrobeat nchini, @harmonize_tz, kuwa wasanii wote wa lebo ya Konde Music Worldwide (@kondegang) hawajawahi pata malipo yoyote ya kazi zao wala ripoti kwa kipindi cha miezi 8. Kutoka kwa kampuni hiyo.

Bosi huyo wa @kondegang kwenye andiko lake alilalamikia kutopata hata senti Tano, ya mauzo ya kazi za wasanii wa lebo yake huku akielekezea kilio chake kwa Serikali akiomba iingilie kati suala hilo.

Mziiki wamesema "@harmonize_tz Ripoti zako hutumwa kwako kila mwezi. Wewe na timu yako @kondegang mnayo sifa za kuingia (login credentials) na mnaweza kupata ripoti wakati wowote. Malipo ya Harmonize Entertainment yanaweza kufanyika mara tu utakapotutumia ankara (invoice) - jambo ambalo hujalifanya na umekataa kulifanya. Tumekushirikisha katika habari zote mpya moja kwa moja kuhusu kuchapisha kazi zako(publishing), na tunasubiri wewe utupe idhini. Tumekuwa tukisaidia uzinduzi wa kazi zako mpya kwa kuweka kwenye playlists kwenye vituo vyote vya kusikiliza muziki mtandaoni (DSPs) kote duniani, kutoa matangazo, miongoni mwa mambo mengine. Unajua tupo hapa kukusaidia wakati wote."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad