Hawa Hapa Mawaziri Walioachwa Katika Mabadiliko ya Baraza



Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Agosti 30, 2023 amefanya mabadiliko Baraza la Mawaziri ambapo Waziri mmoja na Manaibu wawili wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wengine.

Miongoni mwa walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ambaye nafasi yake imechukuliwa na Jerry Silaha Mbunge wa Ukonga.

Pia, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja naye ameachwa huku nafasi hiyo ikichukuliwa na Dunstan Kitandula.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambapo kwa sasa wizara hiyo imegawanywa mara mbili; upande wa Ujenzi Rais Samia amemteua Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri na Uchukuzi amemteua David Kihenzile kuwa Naibu Waziri.


Mabadiliko haya yanatokea ikiwa ni siku 56 tangu afanye mabadiliko madogo katika baraza hilo kwa kuigawa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Ambapo alimteua Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad