Haya Ndiyo yataangaziwa Mazungumzo Ruto na Odinga

Haya Ndiyo yataangaziwa Mazungumzo Ruto na Odinga


Rais wa Kenya William Ruto inadaiwa kuwa amekutana na Kiongozi wa Muungano wa azimio la Umoja Raila Odinga jijini Mombasa siku ya Ijumaa kwa uwepo wa Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo hivyo kuanzisha hatua za mazungumzo zinazohusisha wawakilishi 5 kutoka kila upande.



Bwana Obasanjo ambaye pia akitumwa na jamii ya kimataifa katika zoezi la upatanishi  kati ya Odinga na Rais wa wakati huo wa Kenya , Uhuru Kenyatta mwaka 2018 aliwasili Kenya mwanzoni mwa wiki.


Hatua za mazungumzo hayo yamethibitishwa pia Jumamosi 29 katika tamko la pamoja la miungano ya Azimio la Umoja na Kenya Kwanza.


‘’Sisi uongozi wa muungano wa Azimio la Umoja tumeshauriana na muungano wa Kenya Kwanza chini ya uongozi wa Mheshimiwa Olusegun Obasanjo kuhusu hali ya taifa letu, tumedhamiria kutatua tofauti zetu kwa amani kwa manufaa ya watu wetu wote,’’ taarifa hiyo ilisema.


Katika mazungumzo yanayotazamiwa ni pamoja na kupanda kwa hali ngumu ya maisha, wahanga wa mashambulizi ya polisi na adhabu kwa polisi waliosababisha watu kujeruhiwa na kuuawa.


Timu ya mazungumzo itamuhusisha Kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wah na Kiongozi wa walio wachache bungeni Opiyo Wandayi, wabunge wawili kutoka kila upande na wanachama wawili wasio wabunge kutoka kila upande hivyo kufanya jumla ya wanaohusika kwenye mazungumzo kuwa 10

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad