Huu Hapa Mjengo wa Harmonize anaomjengea Mama yake Mzazi



Rais wa Konge Gang Harmonize ameonesha mjengo wa Ghorofa ambao anamjengea mama yake mzazi. Harmonize ameanika mjengo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao bado haujakamilika.


Harmonize ameambatanisha Video ya mjengo huo na ujumbe huu hapa "Leo sijalewa nimefanya mambo ya msingi sana, hongera mama Konde sinywi tena mpaka nikumalizie kinyumba chako ya dunia ni mengi na walimwengu nao wanaomba Mungu. Muda mwingine nawaza mambo yakikaa vibaya nahamia kwako mama konde, sijalewa na sitolewa tena".

Leo August 15,2023 Harmonize alitangaza kuacha pombe ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka afunguke sekeseke lililopelekea kuachana na aliyekuwa mchumba wake Kajala Masanja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad