JE, Diamond Platnumz Anawanunulia Views Wasanii Aliyoshirikiana nao Kwenye Nyimbo zao, Soma Hizi Takwimu Mtu Wangu Zitakufikirisha zaidi



Kwa miaka kadhaa kumekuwa na dhana au hoja ambayo imekuwa ikitolewa na mashabiki na hata baadhi ya wasanii na wadau wa muziki Nchini wakidai kuwa @diamondplatnumz amekuwa akinunua views ambazo zimemsaidia kuvunja rekodi mbalimbali ikiwemo kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na Kati Kufikisha idadi ya watazamaji Bilioni 1

Je kuna ukweli wowote juu ya hoja hizo? kabla ya kujibu hilo, tazama utafiti huu mdogo unaoonesha nyimbo za baadhi ya wasanii wa Tanzania waliowahi kumshirikisha Diamond Platnumz kuwa ndio nyimbo zilizotazamwa zaidi kwenye Chaneli za #Youtube za wasanii hao

Yaani Msanii yeyote aliyewahi kumshirikisha #diamondplatnumz basi wimbo huo aliomshirikisha Diamond ndio miongoni mwa Nyimbo zake tatu zilizowahi kutazamwa zaidi

Swali ni Je Diamond Platnumz ANAWANUNULIA VIEWS Wasanii Hawa Pia??

#Harmonize - Kwangaru ( 106 Million Views) - Ndio Wimbo Wa Kwanza kwa kutazamwa zaidi kwenye YouTube channel ya Konde Boy

#Mbosso - Baikoko ( 48 Million Views) - Wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi

#Chege - Waache Waoane ( 23 Million Views) - Wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi

#NavyKenzo - Katika ( 29 Million Views) - Wa Kwanza Kutazamwa Zaidi

#Linex - Salima ( 15 Million Views) - Wa Kwanza Kutazamwa Zaidi

#Jux - Sugua ( 12 Million Views) - Wa Kwanza Kutazamwa Zaidi

#Barnaba - Hadithi ( 11 Million Views) - Wa Kwanza Kutazamwa Zaidi

#ProfesorJay - Kipi Sijasikia ( 9.8 Million Views) - Wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi

#FidQ - Fresh Remix ( 3.2 Million Views) -Wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi

#Rayvanny - Tetema ( 76 Million Views) - Ndio Wimbo Wa Pili Kwa Kutazamwa Zaidi

#Rayvanny - Mwanza ( 63 Million Views) - Wa Tatu Kwa Kutazamwa Zaidi

#Zuchu - Cheche ( 35 Million Views) - Wa Tatu Kwa Kutazamwa Zaidi

LIST YA WASANII WA NJE YA TANZANIA👇🏾

#Patoranking - Love You Die ( 61 Million Views) - Wimbo wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi Kwenye YouTube channel ya Patoranking

#MrFlavour - Time To Party ( 117 Million Views) - Wimbo Wa Kwanza Kwa Kutazamwa Zaidi Kwenye YouTube channel ya Mr Flavour

#Waje - Coco Baby ( 2.5 Million Views) - Wa Kwanza Kwa Kutazamwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad