Klabu ya ASAS ya nchini Djibouti imeukubali mziki wa Yanga Sc baada ya kupokea kichapo cha bao 5-1 katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa jana Agosti 26 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mchezaji wa ASAS, Gilbert Kaze raia wa Burundi ambaye amewahi kuichezea Simba Sc msimu wa 2013, amesema Yanga ni timu kubwa hivyo walistahili ushindi.
"Mchezo ulikuwa mzuri, lakini ukweli ni kwamba Yanga ni timu kubwa Afrika, ina wachezaji wengi wenye wazuri na uwezo mkubwa, asilimia kubwa ya wachezaji wake wamekaa pamoja kwa muda mrefu, mechi mbili wamecheza mpira mkubwa na wametuzidi.