Kenya Yaongoza Kuleta Watalii Kwa nchi za Afrika

 


Idadi ya watalii walioingia nchini kipindi cha January hadi Juni 2023 imeongezeka hadi kufikia 759,327, huku Kenya ikiongoza kutoa watalii wengi wanaotembelea Tanzania wakitokea nchi za Afrika.


Hayo yameelezwa leo Agost 9, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu za Kiuchumi nchini, Daniel Masolwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.


Mtakwimu huyo, amesema kuwa Kenya imeleta jumla ya 93,488; huku nchi zingine ambazo wananchi wake wameitembelea Tanzania katika kipindi hicho na idadi yao katika mabano ni pamoja na Burundi (47,418), Rwanda (26,899), Zambia (25, 372) na Uganda (20,727).


Hata hivyo, Masolwa amesema kuwa japo Kenya inaongoza kwa nchi za Afrika, wengi wa watalii hao ametaka nje ya bara la Afrika, huku ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 31.9; ni zaidi ya watalii 575,397 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2022.


“Marekani inaongoza kwa kuingiza watalii wengi (51,674), ikifuatiwa na Ufaransa apmbapo 48,696 kutoka nchi hiyo waliingia Tanzania, huku Ujerumani ikileta watalii 39, 789; huku Uingereza na italia kila moja ikitoa watalii 29,000," amesema.


Hata hivyo, Masolwa anamatarajio makuu, kwani amesema kuwa hadi mwisoni mwa mwaka huu wanatarajia kuingiza mapato zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2022; hii inatokana na hamasa iliyotolewa na filamu ya 'The Royal Tour,' baada ya nchi kukumbwa na janga la uviko - 19 mwaka 2019.


"Mwaka 2022 nchi ilifanikiwa kupata mapato yaliyotokana na utalii kiasi cha dola za Marekani milioni 2,527.8, ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 1,310.3 za mwaka 2021 hivyo mwaka huu tunatarajia yataongeza zaidi," amesema.


Amesema mapato hayo ya mwaka 2022 yalitokana na watalii 1,454,920 huku walioingia nchini mwaka 2021 ni 922,692.


"Idadi ya watalii wengi wanaokuja nchini ni kwa ajili ya mapumziko, wakifurahia zaidi sehemu za wanyama porina fukwe za bahari"


Akizungumzia swala hilo, Mkurugenzi wa ZARA tour, Zainabu Ansell, amesema kuwa ongezeko hilo ni fursa kwa wadau wa utalii kuzidi kuongeza nguvu katika kuhakikisha wanabuni kampeni nyingi za kumuunga mkono Rais Samia, lakini pia mazao mapya ya utalii ili kuleta watalii wengi zaidi nchini.


Amesema kuwa Tanzania ina vivutio vingi ambavyo bado havijatangazwa ipasavyo ili kuvutia watalii wengi zaidi katika kufikia azma ya Serikali ya 2025 ya kufikisha watalii milioni tano, ambao wataliingiza taifa zaidi ya dola bilioni 6.


"Wadau wa utalii na taasisi binafsi na za serikali zinazofanya kazi za utalii yapaswa tushirikiane kuhakikisha vivutio vyetu vinatangazwa, kwani vipo ambazo havijafikiwa, lakini hata vilivyotangazwa, havijakidhi vigezo vya kumvuta mtalii kuweka bajeti mpya kwa ajili ya bidhaa hizo" amesema Ansell.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad