Kimenuka...Namba za 3D Kwenye Plate Number za Magari Zapigwa Marufuku, Polisi Waanza Msako



Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za mbele na nyuma pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Mkuu wa Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi wa Polisi Michael Deleli amesema ni kosa kisheria kufanya mabadiliko na kubadilisha uhalisia kwenye gari kwani huongeza hatari hususan nyakati za usiku.

"Plate number mtu anachukua dukani vizuri kabisa anaiwekea namba zingine, badala ya ile ambayo imechapichwa dukani, lakini ananunua zipo saizi zinachongwa za vioo na herufi zile zinakuwa na ujazo, zote hizo tunafanya oparesheni kuziondoa,” amesema Kamishna.

Ameongeza, “Herufi tu ile inatengenezwa kwa viwango, lakini mtu ameingia tu kati na yeye anaanza kufanya biashara [..] watu waheshimu sheria na kanuni zetu, wasijifanyie kama jinsi wanavyotaka.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad