KIPA Beno Awachimba Mkwara Simba SC Mchezo ngao ya Jamii

 

KIPA Beno Awachimba Mkwara Simba SC Mchezo ngao ya Jamii

Mlinda Lango Beno Kakolanya amesema atahakikisha anafanya vizuri katika timu yake mpya ya Singida Fountain Gate, kama atapangwa kucheza katika mchezo wao wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC.


Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa Agosti 10 katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, Kakolanya amesema atahakikisha anaonyesha kiwango bora na kuisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.


“Najua Simba SC ina wachezaji wazuri kutokana na usajili iliyoufanya, lakini hata timu yetu ina kikosi kizuri mimi na wenzangu tutapambana kuhakikisha tupanata ushindi,” amesema.


Kakolanya anajua baada ya kusajiliwa Singida kibarua chake cha kwanza ni dhidi ya Simba SC aliyotoka, hivyo hatakubali kuona timu yake inapoteza katika mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad