Baada ya kumalizika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kati ya Yanga SC dhidi ya Asas kutoka Djibouti na Yanga kushinda kwa mabao 2-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chamazi Complex.
Kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kocha wa Yanga Miguel Gamondi alitoa ufafanuzi kwanini hakumtumia beki wake wa kati Dickson Job katika mechezo miwili ya Ngao ya jamii kule Tanga lakini amekuja kumtumia kwenye mechi ya kitataifa dhidhi ya Asas.
Swali; Kwanini Dickson Job hakucheza michezo ya Ngao ya Jamii na mchezo dhidi ya ASAS FC umemtumia pale nyuma akiwa na Bakari Mwamnyeto?
Gamondi amesema;
"Unajua watu hawajui kwanini sikumtumia Job kule Tanga, Dickson Job ni mzuri kwenye kucheza mpira tofauti na Ibrahim Bacca ambae ni mzuri kwenye mipira ya juu, Ukiangalia uwanja wa Mkwakwani utaona ulikuwa haumfanyi Dickson Job awe Comfortable kutokana na aina yake ya kucheza mpira wa chini na pasi, ila mmeona pale Azam Complex namna ambavyo amecheza ni mchezaji ambae nitakuwa namtumia kila mechi ninayohitaji kucheza sana mpira maana ana uwezo huo wa kutoa pasi za uhakika hivyo itakuwa vizuri tukicheza kuanzia kwake pale nyuma"