Kocha JKT afunguka kilichomponza akapigwa 5-0 na Yanga

 

Kocha JKT afunguka kilichomponza akapigwa 5-0 na Yanga

Kocha JKT Tanzania, Malale Hamsini amefunguka sababu ya kikosi chake kukubali kupokea kichapo cha bao 5-0 kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga Sc jana katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.


Malale amesema kilichowaponza ni mabadiliko ya wachezaji aliyoyafanya kwani hawakuweza kutekeleza kile ambacho aliwaelekeza kwenda kukifanya ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kuziba njia za yanga kuwaadhibu.


"Mchezo umekwisha, matokeo tumeyakubali. Kilichoniangusha ni zile sub nilizofanya hazikutimiza majukumu yake. Niliwaelekeza wakazibe njia za Yanga lakini sub zangu zimeruhusu njia za yanga kuwa wazi na kusababisha tukafungwa mabao mengi.


"Kipindi cha kwanza njia za yanga nilizizuia kwa viungo na winga zao ambazo wanazitegemea sana. Nilitegemea zile sub zangu zitaendeleza kile tulichokifanya kipindi cha kwanza, lakini wao walipoingia wakataka kurudisha lile bao moja tulilokuwa tumefungwa kipindi cha kwanza, hii ndiyo imegharimu timu nzima.


"Sub zangu zimeniumiza sana, hazikutimiza majukumu yangu kama ambavyo nimewaelekeza, lakini haya ni matokeo ya mpira, tumejua mapungufu yetu ni yapi, tunajipanga kwa mchezo ujao," amesema Kocha Malale.


Kabla ya mechi, Kocha Malale alisema; “Wachezaji wangu nimewaanda kucheza na timu yoyote kubwa kwani Ligi Kuu hakuna timu ndogo. (Yanga) ana wastani wa kufunga mabao 10 ndani ya mechi mbili. Nimeweka viungo wengi lakini kadri mechi itakavyozidi kwenda tutafanya mabadiliko.”


Yanga wameendeleza ubabe wao katika Ligi Kuu kwa kufunga bao 5 kila mechi kwa mechi mbili mfululizo za Ligi na kuwafanya kukaa kileleni mwa ligi wakiwa na alama 6 na mabao ya kufunga 10 bila bao la kufungwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad