KOCHA Mkuu wa Yanga, Agutuka Ubutu wa Kikosi Chake Kuelekea Mechi ya CAF Jumapili, Kufanya Mabadiliko Haya

KOCHA Mkuu wa Yanga, Agutuka Ubutu wa Kikosi Chake Kuelekea Mechi ya CAF Jumapili, Kufanya Mabadiliko Haya


KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amebadilisha program ya wachezaji wake kwa kuwapa mazoezo ya viungo baada ya jana kufanya Gym ili kujiweka sawa kuelekea katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga leo asubuhi walifanya mazoezi ya Gym katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam watakuwa wenyeji wa mchezo huo wa hatua ya awali utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Gamondi alisema kikosi chake kimeanzia amazoezi ya gym kuhakikisha wanakuwa sawa kabla ya jioni kufanya mazoezi ya uwanjani.

Alisema anakazi kubwa ya kuinoa safu yake ya ushambuliaji kuhakikisha anapata mabao mengi katika mchezo huo ili iwe chachu kwenye mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tunaanza na Asas FC tunahitaji matokeo mazuri kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea hatua inayofuata, Wachezaji wako vizuri na katika mazingira mazuri ya kushindana sina wasiwasi na wao kwenye hilo, lakini tunarekebishana zaidi katika nafasi za mbele,” alisema kocha huyo.

Alisema washambuliaji wazuri na wenye uwezo mkubwa, katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, walipata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia jambo amelifanyia kazi kuelekea mechi ijayo anaimani hayatajitokeza.

Kocha huyo alisema kukosa mabao pamoja na kutengeneza nafasi sio sababu ya kuamini kuwa hawawezi kufunga huku akisisitiza kuwa amekaa na wachezaji wake kuwaeleza kutumia kila nafasi wanazotengeneza.

Yanga kesho (Alhamis) itaendelea na mazoezi huku wachezaji wakitoka nyumbani na kesho kutwa (ijumaa) wataingia kambini na tayari kwa mchezo wao dhidi ya ASAS FC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad