Kocha Nabi Aanza Vizuri Morocco Akiwa na FAR Rabat

 

Kocha Nabi Aanza Vizuri Morocco Akiwa na  FAR Rabat

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohammed Nabi ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha FAR Rabat ya Morocco ameanza vyema katika kibarua chake kipya ndani ya klabu hiyo.


Hii ni baada ya FAR Rabat wakiwa ugenini nchini Togo, kuitungua Klabu ya ASKO De Kara kwa kipigo cha bao 1-0 kwenye michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika.


Katika mechi hiyo iliyopigwa jana Agosti 20, 2023 katika Dimba la Stade de Kégué nchini Togo, bao la FAR Rabat lilifungwa na Lamine Diakite dakika ya 18.


Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utapigwa Jumamosi ijayo, AGosti 26, nchini Morocco.


Matokeo mengine;

AS Otoho 1 - 1 Al-Merreikh

ASKO 0 - 1 FAR Rabat

Dragon FC 0 - 2 Big Bullets

Medeama SC 1 - 0 Remo Stars

Coton Sport 0 - 0 ASEC Mimosas

FC Nouadhibou 2 - 0 Al Ahli Tripoli

Hafia FC 0 - 0 Generation Foot

Al Ahli Benghazi 4 - 3 Enyimba

ASAS FC 0 - 2 Yanga.


Habari Zinazofanana:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad