Kocha Wasimba Awatoa Hofu Kuhusu Kiwango cha Luis Miquissone Kushuka 'Nipeni Muda Miquissone Mnaemtaka Atarudi'

Kocha Wasimba Awatoa Hofu Kuhusu Kiwango cha Luis Miquissone Kushuka 'Nipeni Muda Miquissone Mnaemtaka Atarudi'
Luis Miquissone


Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’, amesema kuwa bado anampika kiungo mshambuliaji wake, Luis Miquissone na anaamini atarejea katika ubora wake ambao aliondoka nao Simba mwaka 2021.

Robertinho amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji ambapo Simba waliibuka na ushindi wa bao 2-0.

Miquissone amesajiliwa na Simba baada ya kumalizana na klabu yake aliyokuwa akiitumikia, Al Ahly ya Misri huku kiwango chake kikitajwa kuporomoka tofauti na alivyokuwa wakati akiwa Simba miaka michache iliyopita.

“Tukiwa kwenye kambi Uturuki nilikuwa namtumia Luis Miquissone kwa kucheza dakika 25 kisha dakika 30 na sasa namtumia kwa dakika mpaka 40.

“Sio rahisi lakini nafurahi kumuona kwa sababu Luis ana kipaji cha hali ya juu sana. Nitamtumia sana tu huko mbele na pengine baada ya siku 15 nitakuwa namwanzisha kila mara,” amesema RObertinho.

Kwa sasa Miquissone amecheza michezo kadhaa ya Simba akifanikiwa kutengeneza bao moja (assist) aliyompa Clatous Chama akafunga bao la 3 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad