Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth
Magomi amesema Mawe hayo ya madini yamekamatwa katika msako maalum uliofanyika Julai 26 hadi Agosti 22 Mwaka huu baaada kufanyika kwa msako maalum.
Sambamba na hilo ieshi hilo lilikamata Carbon yenye mchanga wenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenve uzito wa kg 261 ambayo thamani yake bado haijajulikana katika maeneo ya Manzese Kahama.
Tumefanikiwa kukamata jumla ya lita 603 za mafuta aina ya Diesel katika maeneo tofauti ya mradi wa Reli ya mwendokasi SGR. Mafuta haya yamewekwa kwenye chupa ndogo, wezi wa mafuta sasa hivi wamebuni mbinu ya kutumia vichupa badala ya madumu makubwa" amesema Kamanda Magomi.