Maambukizi Mapya ya VVU kwa wasichana yaongezeka

Maambukizi Mapya ya VVU kwa wasichana yaongezeka


Hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hapa nchini kwa vijana imezidi kuongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya maambukizi mapya ya VVU ni vijana wa kiume huku asilimia 80 ni kwa vijana wa kike 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa uragibishi na habari kutoka TACAIDS Jumanne Isango, na kusema mazingira ambayo yanapelekea vijana kupata VVU zaidi ni mimba za utotoni na kutotumia kinga, hivyo wanachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wale wenye VVU wanaendelea kutumia dawa za kufubaza makali.


"Hali ya VVU kwa sasa kwa vijana sio nzuri na hii inasababisha maambukizi kuendelea kuwa makubwa kwani wengi wao hawatumii kinga,'' amesema Mkurugenzi huo


Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU nchini Deogratius Peter Rutatwa, amesema maambukizi ya VVU kwa vijana kuwa makubwa ni kutokana na wazazi kwenye ngazi ya familia kutozungumza na vijana wao juu ya elimu ya afya ya uzazi ama wazazi kutotoa kipaombele cha elimu ya masuala ya kujamiiana 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa vijana wanaoishi na VVU nchini Pudenciana Ngwiliza, amewashauri vijana kupima afya zao na wanapobainika kwamba wamepata maambukizi wasione aibu wajitokeze hadharani na kuungana na wenzao Ili kuanza matumizi ya dawa za kufubaza makali ya ukimwi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad