MABOSI wa Simba wajanja sana, Kufanya Utambulisho wa Makipa Hawa Wapya, Mmoja Kutoka Ufaransa



MABOSI wa Simba wajanja sana, wakati leo ni Simba Day, wenyewe wamepanga kuwafanya sapraizi mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwatambulisha makipa wawili wapya akiwamo aliyecheza soka lake lote Ulaya, licha ya kuwa na uraia wa DR Congo 🇨🇩 Lionel Mpasi Nzau

Kipa huyo mwenye urefu wa futi sita na mzaliwa wa mji wa Meaux, Ufaransa amesajiliwa kutoka klabu ya Daraja la Pili ya Ufaransa iitwayo Rodez AF, huku pia akiidakia timu ya taifa ya DR Congo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinasema kipa huyo aliyewahi kucheza timu ya vijana za PSG U-19,

Toulouse pamoja na timu za taifa za vijana za Ufaransa U16, U17 na U18 amepewa miaka miwili na leo atatambulishwa rasmi sambamba na kipa mzawa Hussein Abel aliyewahi kuichezea KMKM, tanzania Prisons na KMC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad