Matokeo Azam FC Vs Tanzania Prisons Ligi Kuu Tanzania Bara


Matokeo Azam FC Vs Tanzania Prisons Ligi Kuu Tanzania Bara

Matokeo Azam FC Vs Tanzania Prisons Ligi Kuu Tanzania Bara


Baada ya kutupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya awali, kikosi cha Azam Fc leo kina mtihani mwingine mbele ya Tanzania Prisons



Ni katika mchezo wa ligi kuu ya NBC mzunguuko wa pili ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi



Pengine hii itakuwa mechi muhimu sana kwa Azam Fc kushinda ili kurejesha imani ya mashabiki wao ambao bado hawaamini kile kilichotokea pale uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Fasil Dar Kenema ya Ethiopia



Hata hivyo wanakutana na Tanzania Prisons inayonolewa na Kocha Fred Felix Minziro aliyejiunga na timu hiyo akitokea Geita Gold



Prisons walipata alama moja muhimu katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Singida FG mchezo ukipigwa uwanja wa LITI mkoani Singida



Ushindi leo unaweza kuirejesha Azam Fc kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Kitayosce Fc

MATOKEO

AZAM 3:1 TANZANIA PRISONS

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad