MATOKEO Simba vs Singida Fountain Gate Leo 10 August 2023

 

MATOKEO Simba vs Singida Fountain Gate Leo 10 August 2023

Mnyama Mkubwa Mwituni. Simba SC itakuwa ikishuka dimbani kuwakabili Singida FG FC katika dimba la Mkwakwani pale jijini Tanga.


Simba ambayo imesheheni wachezaji mafundi kama vile Onana, Baleke, Kramo, Mwalimu Fabrice Ngoma na wengineo wanatarajiwa kutoa burudani kubwa sana kwa wapenda kandanda nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla mara baada ya butua butua na piga nikupige ya jana.


Singida ambayo imefuzu kucheza kimataifa nayo imesajili wachezaji kadhaa akiwemo Kiyombo, Babu Onyango, Yahaya Mbegu na wengineo wanatarajiwa kuleta ushindani.


Ewe mwana Simba uliyepo Kasulu, Jinja, Makambako, Kisumu, Uyui, Ndola, na mahala popote tegemea mpira mkubwa leo na mechi yenye mvuto.


Mechi itapigwa Saa 1:00 Usiku na itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD

MATOKEO SIMBA VS SINGIDA FOUNTAIN GATE

FULL TIME: SIMBA 0:0 SINGIDA FOUNTAIN GATE


PENALT

SIMBA 4

SINGIDA 2


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad