Matokeo ya Simba vs Mtibwa Sugar NBC Premier League Leo 17 August 2023

 

Matokeo ya Simba vs Mtibwa Sugar NBC Premier League Leo 17 August 2023

Kikosi Cha Simba kinatarajia kuingia uwanjani kesho dhidi ya Mtibwa sugar, mkoani morogoro uwanja wa Manungu Complex.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 Jioni  

Klabu ya Mtibwa Sugar imethibitisha kuwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utapigwa Uwanja wa Manungu, Turiani

Awali kulingana na taarifa iliyokuwa imetolewa na Mkuu wa mkoani wa Morogoro Mh Adam Malima, jitihada zilikuwa zikifanyika mchezo huo uhamishiwe uwanja wa Jamhuri

Mchezo utapigwa kesho Alhamisi, August 17 majira ya saa 10 jioni

Simba itakwenda huko kwenye mashamba ya miwa ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho uliopigwa msimu uliopita

Jean Baleke alifunga hat-trik na kuondoka na mpira katika mchezo huo ambao Simba ilitumia dakika 45 tu kuiangamiza Mtibwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ametamba kuwa msimu huu watahakikisha wanaondoka na alama tatu katika kila mchezo

"Tunahitaji alama tatu kwenye kila mchezo ili tutimize malengo yetu ya kutwaa ubingwa mapema," alisema

MATOKEO


FULL TIME: SIMBA 4:2 MTIMBWA SUGAR

Goals Simba

Baleke

Onana

Ngoma x2

Goals Mtibwa

M. Anthony x2


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad