Mayele Afichua Siri: Nabi na Kaze waliondoka na mabegi yao yote mechi ya Africain

Mayele Afichua Siri: Nabi na Kaze waliondoka na mabegi yao yote mechi ya Africain


Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele amefichua kuwa, aliekuwa Kocha wao Nasreddine Nabi pamoja na msaidizi wake, Cedric Kaze, walifungasha mabegi yao kabisa wakati wanakwenda kucheza mechi dhidi ya Club Africain.


Mayele ameyasema hayo kupitia documentary ya Yanga iliyozinduliwa hapo jana Agosti 7, 2023 ambapo mechi hiyo ya msimu uliopita wakati Yanga wakishiriki mashindano ya Shirikisho Afrika, ilikuwa imebeba hatma yao na endapo wangepoteza basi wangetolewa kwenye mashindano.


“Wakati tunaenda kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Club Africain, Kocha Kaze alifungasha mabegi yake yote akamwambia mke wake tukirudi tunarudi Burundi.


“Kocha Nabi naye aliondoka na Mabegi yake yote halafu tukawa tunasikia kuwa kuna Kocha mpya,” Mayele akizungumza kwenye Documentary ya Yanga Sc.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad