Wakati Simba ikitoka na ushindi wa mabao 4-2 mbele ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro.
Wachambuzi wengi wa michezo wamezungumzia kiwango cha beki wa kati wa Simba Che Fondoh Malone ambae jana alionekana kufanya makosa mengi yaliyoigharinu simba.
Mmojawapo ni Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3, Alex Ngereza ambae anazungumzia kiwango cha mchezaji huyo.
Alex Ngereza anasema;
“Che Malone sio beki wa kumtegemea sana hana speed ya kutosha hata goli la pili ambalo wamefungwa na Mtibwa Suger limetokana na makosa yake ametoka kwenda kushambulia akachelewa kurudi”
ROBERTINHO NAYE KAGUNA..
Katika hatua nyingine Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema bado anaitengeneza timu yake ili kuhakikisha anakuwa na kikosi imara.
Aakizungumza mara ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa kumalizika na timu yake kuibuka na ushindi wa 4-2, Robertinho alisema, amejaribu kuwatumia wachezaji wake karibu wote ili aweze kuwaingiza mchezoni.
“Nimewatumia kina Chama, Baleke, Luis, na wengine ili tutengeneze timu nzuri na namshukuru Mungu tumepata matokeo na nawapongeza wachezaji,” alisema Robertinho.