Mikopo Kausha Damu Chanzo Ndoa Nyingi Kuvunjika Mitaani


Mikopo umiza inayotolewa na watu binafsi mitaani imetajwa kuwa chanzo Cha ndoa nyingi kuwa hatarini kuvunjika kutokana na baadhi ya Wanawake kuweka dhamana vitu vya ndani ikiwemo hati za Nyumba na vinginevyo

Wakizungumza Wanawake wa Manispaa ya Shinyanga wamesema changamoto kubwa ni Mikopo umiza wanayochukua mitaani ambayo inasababisha wengi kuingia kwenye matatizo ya Kifamilia

Kwa Upande wake,Mbunge Viti maalum Shinyanga Salome Makamba wakati akiwatembelea Wakina Mama hao katika Maeneo Yao amesema wengi wamekua wakifuata mikopo hiyo kwakua ni nafuu Lakini huishia vilio

Nae Mkazi Wa Manispaa Shinyanga Mariam Senkondo amesema Mikopo Umiza imekua Janga Kubwa Kwa Wanawake kutokana na wengi wao kushindwa kulipa marejesho na familia kuingia hatiani

"jamani Wakina mama tuna wakati mgumu sana tunapenda mikopo Ili tufanye biashara Lakini inatuumiza wengine wanaita Kausha damu Sasa ukifikiria kwenda Benki masharti ni magumu zaidi ni Bora tufie hukuhuku"

Aidha,Wanawake hao wameiomba Serikali kuangalia pamoja na kuwadhibiti watu wanaofanya biashara ya kukopesha fedha na kutoza Riba kubwa ambayo imekua kama njia ya kuwakandamiza wenye kipato Cha chini .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad