Mtoto wa Mwaka Mmoja Agongw na Lori na Kufariki Wakati Likirudi Nyuma





Mtoto wa mwaka mmoja alikanyagwa hadi kufa katika eneo la kuegesha magari eneo la Dandora, jijini Nairobi.

Polisi walisema dereva wa lori alikuwa akirudisha gari nyuma kutoka sehemu ya kuegesha wakati ajali hiyo ilipotokea.

Mtoto huyo alikuwa akirandaranda nyuma ya lori hilo na dereva hakujua wakati alipoingia kuliwasha ili kuondoka.

Kulingana na polisi, lori hilo lilimgonga na kumkanyaga mvulana huyo katika tukio hilo la Jumatano.


Majirani walioshuhudia tukio hilo la kusikitisha walipiga yowe katika jaribio la kumfahamisha dereva bila mafanikio.

Tukio hilo lilitokea wakati dereva alikuwa akiondoka kuelekea kazini mwendo wa saa mbili asubuhi, polisi walisema.

Mwili wa mvulana huyo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Mama Lucy ukisubiri uchunguzi wa upasuaji huku lori hilo likizuiliwa kwa ukaguzi.


Huku hayo yakijiri, ombaomba aliuawa na umati baada ya yeye na mwanamume mwingine kumpiga hadi kumuua mwenzake katika mabishano ya pesa katika eneo la Roasters, Nairobi.

Polisi walisema kisa hicho kilitokea katika Mto wa Alsops, ambapo wazururaji wawili wa kiume wanaoaminika kuwa marafiki wakubwa na rafiki yake walimuua mwathiriwa aliyetambulika kwa jina la Ben.

Kundi la watu waliokuwa na hasira lilimzunguka mmoja wa washukiwa hao alipokuwa akijaribu kutoroka eneo la tukio na kumpiga hadi kufa.

Polisi walifika hapo muda mfupi baadaye, walichukua miili na kuipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Polisi wanaoshughulikia kesi hiyo walisema wanawasaka washukiwa wengine waliohusika katika mauaji hayo.

Wapelelezi walisema wamebaini kuwa kundi hilo lilitofautiana kuhusu jinsi ya kugawana mkusanyo wa siku hiyo na kusababisha kipigo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad