Mume Ampasua Mkewe Kichwani kwa Shoka na Kufariki


Mume ampasua mkewe kichwani kwa shoka na kufariki papo hapo kisa kuletewa wito rasmi wa mahakama kuhusu talaka

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi nchini Zambia, mume kwa jina la Victor Sungababwa(43) alimuoa Atrina(33) kuwa mke wa pili mwaka 2013 lakini kufikia 2015 ndoa yao ilikuwa ishakumbwa na migogoro wakawa wanaishi hivyo hivyo tu kwa kuvumiliana

Hata hivyo, baada ya miaka hiyo ndani ya ndoa, mwezi huu mke yalimfika shingoni akaamua kukimbilia mahakamani ili apewe talaka yake rasmi aendelee na maisha yake mengine

Tarehe 27 mwezi huu August mke alipokuwa akimpelekea mume wake taarifa rasmi ya mahakama kuhusu talaka yake, mume alikataa kusikiliza, baadaye mume alimuita mwanahabari akamwambia aje kuwa shuhuda kuhusu suala hilo lakini wakati wapo nje , mume aliingia ndani ya nyumba akarudi na shoka akiwa amelificha kwa nyuma mgongoni ghafla akalitoa na kumpiga nalo kichwani mkewe na kumpasua kichwani akaanguka na kufariki papo hapo

Mume akakimbilia ndani kunywa kimiminika chenye sumu kwa lengo la kujiua na yeye hata hivyo amewahiwa kuokolewa na sasa anaendelea vizuri hospitalini akisubiri kusomewa mashtaka yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad