Rais Yoweri Museveni ametoa kauli hiyo baada ya WB kutangaza kusitisha Ufadhili na Mikopo yote mipya iliyoombwa na Serikali kutokana na Nchi hiyo kupitisha Sheria inayozuia Mapenzi ya Jinsia moja
Museveni amesema "Inasikitisha kuona Benki ya Dunia na wahusika wengine wanathubutu kutulazimisha kuacha Imani, Utamaduni, Kanuni na Uhuru wetu kwa sababu ya Pesa. Hatuhitaji shinikizo kutoka kwa yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo yetu."
Hata hivyo, kiongozi huyo amesema Uganda itaendelea na majadiliano na Benki ya Dunia ili kuangalia namna bora ya kuondoa mkanganyiko uliopo.