Mwamba Ajichoma Moto Hadharani Watu Wakishuhudia Kisa Ugumu wa Maisha



Mtu mmoja mkazi wa Kaunti ya Mombasa, amelazwa katika Hospitali Kuu ya Pwani nchini Kenya baada ya kupata majeraha kufuatia kujijijeruhi kwa moto akikusudia kujiuwa kutokana na ugumu wa maisha.

Manusura huyo, ambaye anadaiwa kuwa ni mkazi wa Kaunti ya Kiambu, alifika katika mzunguko wa duka kuu la Naivasha na kujichoma mbele ya umati uliokuwa ukipita na kushuhudia tukio hilo.


“Alikuwa akilalamikia gharama ya juu ya maisha kabla ya kutekeleza kitendo hicho. Alianguka chini kutoka jirani na mnara baada ya kuungua kwa muda,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Hata hivyo, inadaiwa mtu huyo alikuwa amehitimu Chuo Kikuu cha Nairobi, na alipotezana na familia yake iliyochapisha tangazo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook wiki iliyopita ikisema kwamba inamtafuta.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad