Mwamba Aliyemuua Mpenzi Wake Porini Mbele ya Mwanae Kisa Kuachwa Akamatwa na Polisi


Mwamba Aliyemuua Mpenzi Wake Porini Mbele ya Mwanae Kisa Kuachwa Akamatwa na Polisi


Samwel Nduluhundu (38) Mkazi wa Mtaa wa Ramadhani Mjini Njombe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la mauaji ya Felister Danda (24) ambae alikutwa ameuawa Ijumaa iliyopita na mwili wake kutelekezwa katika msitu wa kupandwa wa TANWAT huku Mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili akiwa hai karibu na mwili wa Mama yake.


RPC wa Njombe John Makuri amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo Ferister Danda na Mtuhumiwa Samwel Nduluhundu walikuwa Wapenzi lakini baadae marehemu aliamua kukataa kuendelea na mahusiano hayo “Samwel hakukubaliana na maamuzi ya Felister na kumtaka amrudishie vitu ambavyo amewahi kumnunulia ambapo nae alikataa kurudisha akimwambia hata yeye amemtumia”


Kamanda Makuri amesema jibu hilo lilimfanya Mtuhumiwa baada ya siku kadhaa kumrubuni Felister kwa kumshauri ampeleke kwa Mtaalamu wa tiba asili Wilaya ya Wanging’ombe kwa usafiri wa pikipiki akatibiwe ugonjwa aliokuwa nao eneo la shingo uliokuwa ukimsumbua muda mrefu ambapo Felister alikubali”


“Alhamisi usiku Mtuhumiwa alimchukua nyumbani kwake Felister akiwa na Mtoto wake ambaye alizaa na Mwanaume mwingine sio Samwel na wakaelekea Wanging’ombe lakini walipofika eneo la msitu ndipo inadaiwa alitekeleza mauaji hayo”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad