Mwamposa na Kanisa Lake Wamkosesha MC Pili Pili Usingizi Aliyeanzisha Kanisa na Waumini Watano Pekee

 

Mwamposa na Kanisa Lake Wamkosesha MC Pili Pili Usingizi Aliyeanzisha Kanisa na Waumini Watano Pekee

Mchekeshaji maarufu nchini na mwanzilishi wa Kanisa la Upendo (Love Church) lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam amesema kuwa alianza na waumini watano pekee lakini kwa sasa kanisa lake linaendelea kukua.


Mshereheshaji huyo ambaye pia kabla ya kuanza sanaa ya uchekeshaji, aliwahi kuwa mwalimu amesema malengo yake ni kuja kuwa na kanisa kubwa kama la mchungaji Boniphace Mwamposa wa Kanisa la Inuka Uangaze (Arise and Shine Church).


"Wakati nafungua Kanisa langu nilianza na waumini tano, lakini mpaka sasa nina waumini 50 na lengo langu ni kuwa na waumini wengi kama Mwamposa. Ninajua nitafika, japo itanichukua muda mrefu kufika.


"Watu wengi wanadhani nimekurupuka tu kuwa mchungaji, mimi nimezaliwa na damu ya uchungaji tangu nikiwa mdogo nilikuwa nahudumu kanisani na shuleni na nilianza kuitwa Mchungaji nikiwa mdogo kabisa," amesema MC Pilipili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad