Mwanaume Aliyejitekeza Kwa Moto Kisa Ugumu wa Maisha Kenya Afariki Dunia


Mwanamume aliyejulikana kwa jina Robert Gituhu aliyejiteketeza kwa moto Siku ya Jana (Alhamisi) akilalamikia ugumu wa maisha alifariki saa Nne na Dakika 20 Usiku wa Jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Pwani, Coast General nchini Kenya.

Msimamizi Mkuu wa Coast General Iqbal Khandwalla amethibitisha kwamba mwanamume huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 alipata asilimia 80 ya majeraha ya moto na kwamba alifariki siku iyo hiyo aliyolazwa hospitalini.

“Madaktari wetu walifanya kila wawezalo, tulimpa dawa na matibabu mengine yaliyofaa, lakini kwa bahati mbaya alifariki saa nne na dakika 20 usiku,’ amesema Bw Khandwalla.

Kwenye video iliyosambazwa mtandaoni mwanamume huyo alionekana akiwa amebeba bendera ya Kenya kabla ya kujiwashia moto katika eneo la Mwembe Tayari, Kaunti ya Mombasa.

Marehemu alikuwa mhitimu wa Chuo Kikuu cha Nairobi. Alisomea taaluma ya uhandisi ambapo alihitimu mwaka 2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad