Mwijaku Amshukia Shilole "Naujua Uchafu Wako Mwingi Usitake Niseme Mkagombana na Mume Wako"



@mwijaku amemuonya @officialshilole baada ya Shishi kumtaka Mwijaku amuombe radhi mwimbaji na Malkia wa muziki wa Taarab nchini, @officialkhadijakopa baada ya kutupiana maneno mazito hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii.

Shishi ameandika; "Mama Khadija ni mwanamuziki ambae mimi nimeanza kumsikia toka mdogo kwetu Igunga mpaka leo mimi ni msanii. Ni Mama ambae sisi wanamuziki wa kike tuna muangalia na kutamani uwezo alionao Toka msichana mpaka leo mama na wajukuu".

"Kiukweli Unapo mkosea heshima huyu mama ni Sawa na kutukosea heshima wanawake na Sio wanawake tu Bali Hata Mila na tamaduni zetu zimetuasa kuheshimu wakubwa. Sijpenda ulichofanya ndugu yangu MWIJAKU naomba umuombe radhi mama Khadija Kopa. @officialkhadijakopa".

Ndipo Mwijaku akaibuka na andiko hili, "Shishi tafadhali sana, usilazimishe niseme mauchafu yako. Mwisho mkagombana na mumeo. Unajua kuwa naongea uongo kwa mumeo kila anapotaka kujua habari zako, tafadhali nakuheshimu basi niheshimu usinitaje kwenye mambo yako ya kipuuzi".

"Nimekaa na wewe siku Saba (7), nimejua tabia zako zote, tuheshimiane tafadhali".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad