Paul Kagame Amteua Mwanaye Mrembo Kufanya Kazi Ofisi ya Rais



Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemteua Binti yake Ange Kagame (29), kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Sera na mikakati katika ofisi ya rais, uteuzi ambao unakuja kufuatia azimio la Baraza la mawaziri uliofanyika katika Kijiji cha Urugwiro.

Ange Kagame, msomi wa Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Columbia atakuwa akimshauri baba yake (Rais Kagame), kuhusu sera na mikakati muhimu ya kiuchumi na kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa Mchambuzi Mkuu wa Sera katika ofisi hiyo ya Rais.


Paul Kagame na Bintiye Ange. Picha ya Pulse.
Binti huyo, anaungana na ndugu zake ambao tayari wanaunda kundi la ndani la rais baada ya Januari mwaka huu, 2023 mtoto mwingine wa Kagame, Ian Kagame kuidhinishwa katika kundi la Walinzi wa Rais, baada ya kuhitimu Chuo cha Kijeshi cha Sandhurst Royal Military.

Aidha, miaka ya hivi karibuni, pia Ivan Kagame ambaye ni mtoto mkubwa wa Rais Kagame alipewa nafasi ya kujiunga na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, kitu ambacho kinafanya Kagame kufananishwa na mshauri wake Yoweri Museveni ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kuteuwa wanafamilia katika nyadhifa muhimu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad