Phiri Afunguka Haya Kuhusu Penati Aliyokosa Kwenye Ngao ya Jamii

 

Phiri Afunguka Haya Kuhusu Penati Aliyokosa Kwenye Ngao ya Jamii

Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa amechelewa kuchapisha picha akiwa na Ngao ya Jamii kwakuwa alitingwa katika kuutafuta mpira uliopotea Usiku wa jana katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga dhidi ya Yanga.

“Pole jamani nimechelewa kwa sababu nilienda kutafuta mpira nilioukosa jana. Firstly Thank you to all Simba fans who celebrated with us yesterday night good effort to all the players including the board members who came through asanteni” Ameandika Phiri.

Itakumbukwa mara baada ya kutamatika dakika 90 ya fainali ya Ngao ya Jamii mchezo huo uligeukia katika changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba iliibuka ushindi wa penati 1-3.

Kwa matokeo hayo Simba imetawazwa kuwa bingwa mpya wa Ngao ya Jamii na kufikia rekodi ya Yanga ya kubeba taji hilo mara Saba

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad