Rais Ruto Awapigania Watengeneza Mauzui Mtandaoni Kutoka Kenya, Sasa Kuanza Kulipwa


Rais William Ruto wa Kenya ametangaza kuwa mitandao miwili ya kijamii imekubali kuwalipa Watengeneza maudhui (Content Creators) kutokana na maudhui wanayotengeneza nchini humo kufuatia mazungumzo ambayo amefanya na Viongozi wa mitandao hiyo.

Ruto amesema hayo Ikulu jana wakati wa kuzindua Tamasha la Muziki la Kenya ambapo miongoni mwa Kampuni hizo ni Facebook ambayo imekubali kufanya majaribio kwa Content Creators 25 wa Kenya ili kuona jinsi maudhui yao yanaweza kutengeneza mapato.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja nimejadiliana na Wamiliki wa mitandao ya kijamii kuanzia Facebook, Twitter, TikTok hadi Youtube na tukaendeleza mazungumzo yetu” —— Ruto.

Kauli ya Ruto inakuja wiki chache baada ya Elon Musik kuanza kuwalipa Watumiaji wa mtandao wa X (zamani Twitter) kutokana na maudhui yao ikiwemo posts za kawaida na video na kupokea sehemu ya mapato yanayotokana na matangazo ambapo waliolipwa ni wenye kwa akaunti ambazo zimejisajili kwenye Twitter Blue (X Premium) pekee na zenye views zaidi ya milioni 5 kwa kila chapisho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad