Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo
"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia